Idadi ya tembo nchini Kenya imeongezeka lakini simba wanapungua huku duma wakiwa katika hatari ya kuangamia. Kwenye orodha ya mataifa ya Afrika yaliyo na ndovu wengi zaidi, Kenya ni ya nne baada ya Zimbabwe, Botswana na Tanzania kuipiku. Kwenye makala ya Mtu na Mazingira, Thelma Mwadzaya anaangazia sensa ya kwanza ya kitaifa kuwahi kufanywa ya wanyama nchini Kenya.