JangaMauritius
Mauritius yatoa tahadhari ya kimbunga Belal
16 Januari 2024Matangazo
Kimbunga Belal kimesababisha maelfu ya watu kukosa umeme na magari kadhaa kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.
Polisi wameripoti kuupata mwili wa mwendesha pikipiki katika barabara kuu iliyofurika.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mauritius ulikuwa umefungwa jana Jumatatu (15.01.2024) huku shirika la ndege la nchi hiyo likitangaza kufuta safari kadhaa za ndege zilizopangwa leo Jumanne.
Februari mwaka jana, Mauritius ilikumbwa na mvua kubwa na upepo mkali kutokana na kimbunga Freddy, ambacho kilisababisha wimbi la vifo na uharibifu katika nchi za kusini mashariki mwa Afrika zikiwemo Malawi, Msumbiji na Madagascar.