Merz:Ulaya ijiandae na uwezekano wa Trump kurejea madarakani
27 Julai 2024Matangazo
Merz amesema Ulaya inapaswa kujiandaa licha ya kuwa kwa sasa ushindani ni mkali wa kuwania urais wa Marekani baada ya rais Joe Biden kujiengua na kumuachia nafasi yake Kamala Harris.
Mwanasiasa huyo wa chama cha Christian Democratic Union, CDU ameyasema hayo katika mahojiano yaliyochapishwa leo Jumapili, na kuongeza kuwa Ulaya ilipaswa kufanya hivyo miaka minane iliyopita, akisisitiza kuwa ikiwa atashinda, Trump atakua amejiandaa vilivyo kushikilia wadhifa huo.
Ujerumani pamoja na mataifa mengine ya magharibi ambayo ni washirika wakuu wa Marekani wamekuwa na hofu ya kurejea kwa Trump madarakani kutokana na misimamo ya kiongozi huyo hasa kuhusu masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na kijeshi.