Mfahamu Björn Höcke wa AfD
10 Februari 2020Mgombea huyo alipata ushindi. Lakini alijivua cheo chake muda mfupi baadaye. Hata hivyo mwiko wa kutofanyakazi na AfD umevunjwa. Nyuma ya mipango ya AfD kwa hakika ni kiongozi wa chama hicho wa jimbo la Thuringia, Björn Höcke ambaye hutengeneza makundi kwa kuwagawanya watu.
Hili lilithibitika mnamo mwezi Oktoba wakati wa kampeni muda mfupi kabla ya uchaguzi wa jimbo HILO: Anapotokea Höcke appears, kelele zinazidi. Hili halina ubishi. Baadhi ya watu hupiga makofi na "Höcke, Höcke, Höcke", na wengine hupiga miluzi na kutamka kwa sauti ya juu "Wanazi waondoke”
Ufa huu unaonekana pia katika mji wa Bad Langensalza katika jimbo la mashariki mwa Ujerumani la Thuringia. Na Björn Höcke anaonekana kufurahia hali inavyozidi kutokota. Wakati anapopanda jukwaani ananyanyua mikono yake kuwasalimu wafuasi wake kwa tabasamu ambalo halitoweki katika hotuba yake ya saa moja.
Höcke anaigawa Ujerumani?
Ni hakika kuwa Höcke ni mwanasiasa anayeigawanya zaidi Ujerumani. Katika chaguzi za majimbo mnamo Oktoba 27, alikiongoza chama chake kupata zaidi ya asilimia 23 za kura kama mgombea mkuu wa AfD: Hili linakifanya chama hicho cha siasa kali za mrengo wa kulia kuwa chama cha pili chenye nguvu zaidi kwenye bunge la jimbo la Thuringia. Hata hivyo kura za maoni za uchaguzi wa awali zilionesha kuwa ni asilimia nane pekee ya wakaazi wa jimbo hilo ambao wangempigia kura Höcke iwapo Waziri mkuu wan chi angekuwa akichaguliwa moja kwa moja na raia.
Mwanasiasa huyo ambaye ana siasa kali za mrengo wa kulia amewaweka kiganjani marafiki zake katika chama. Ni mtu ambaye alisababisha mabadiliko katika siasa, mabadiliko ambayo yanajumuisha maneno kama "kuzorota” au "ushindi kamili” kwenye hotuba zake ingawa kama mwalimu wa zamani wa historia anafahamu ni sura ipi ya historia ya Ujerumani anayoiwakilisha.
Alaumiwa kwa ubaguzi
Mtafiti wa siasa za mrengo wa kulia wa mjini Jena Axel Salheiser anasema lugha anayotumia Höcke na wawakilishi wa chama chake cha AfD imejaa maneno ambayo yanafanana sana na yale yaliyokuwa yakitumika wakati wa utawala wa kinazi.
Katika jukwaa dogo huko Bad Langensalza, Höcke anajua namna ya kuwafanya watu wapige makofi katika meza zao wakati wakinywa pombe. Wengi katika eneo hili hawaridhishwi na sera ya uhamiaji ya kansela Angela Merkel, hasa uamuzi wake wa mwaka 2015 wa kufungua mipaka na kuwaruhusu mamia kwa maelfu ya wahamiaji kuingia Ujerumani.
Wengi pia wanalalamika kuwa vyama vya siasa havitilii maanani wasiwasi wao. Kumwita Kansela Merke kuwa ni "kiongozi wa utawala " kukosoa wasomi wa nchi” na kuviita vyama vingine "magenge ya wahuni ” kama anavyofanya Höcke, yote haya yanakubalika katika mji wa Bad Langensalza
Moja ya viungo muhimu katika mafanikio ya Höcke ni kucheza na ubaguzi wa rangi. Wakati mwingine anawataja waafrika wote kama "Aina ya Waafrika wanaozaliana hovyo ” Na wakati mwingine analalamika kuwa maelfu ya vijana wa kijerumani wanakabiliwa na hofu kwa sababu huchokozwa, kuteswa na kupigwa wahamiaji.
Si wengi waliofika katika kampeni zake kwenye mji huo wanakubaliana na matamshi yake lakini wengi hawataki pia kumlaumu. Mmoja wa afuasi wake anasema ni kweli kiongozi huyo anapaswa kuacha kutumia matamshi hayo hasa katika kipindi cha kabla ya uchaguzi vinginevyo matamshi yake yapo sahihi.
Mjini Bad Langensalza, Höcke hana wafuasi pekee lakini pia watu ambao wanakasirishwa na utendaji wake. Mmoja wao ni mchungaji Dirk Vogel ambaye anakasirika kuwa AfD ilichagua kanisa lake kuwa mahali pa kampeni za uchaguzi.
Kwa mtazamo wa mchungaji huyo, Hocke anawagawanya, na kuwawekea ukuta wa tamaduni nyngine. Höcke huzungumza kwa nadra sana na vyombo vya habari. Kabla ya uchaguzi wa jimbo, hakufanya mahojiano yoyote kando ya yale aliyoyakacha katikati na televisheni ya ZDF.
Alimaliza mjadala na televisheni hiyo kwa kusema huenda akawa mwanasiasa mzuri zaidi Ujerumani. hili yawezekana likawafurahisha baadhi ya watu na kwa wengine likawa mithili ya ndoto mbaya.