SiasaMarekani
Bunge la Marekani laidhinisha azimio la mshikamano na Israel
26 Oktoba 2023Matangazo
Hatua hiyo iliyopewa jina "Kusimama na Israel inapojilinda dhidi ya vita vya kikatili vilivyoanzishwa na Hamas na magaidi wengine," ilipata uungwaji mkono wa karibu wabunge wote wa Republican na Democrats. Hata hivyo wabunge 10 wa Democrats hawakupiga kura.
Spika Johnson, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Republican kutoka Louisiana, katika hotuba yake ya kukubaliwa na bunge alisema jambo la kwanza atakalofanya ni kuwasilisha muswada huo wa kuisaidia Israel.
Johnson, alikuwa ni mgombea wa nne ndani ya mwezi huu kuteuliwa kuwania kiti cha uspika, ambacho kimekuwa wazi tangu tarehe 3 Oktoba baada ya Kevin McCarthy kupinduliwa na wajumbe wa chama chake walioasi.