Michezo ya redio kuhusu Elimu ya Kidijitali Afrika
8 Julai 2024Binamu hawa watatu; Jennifer, mtu mwenye ushawishi mitandaoni, Rahim, gwiji wa teknolojia, na Faith, mwalimu anayeipenda kazi yake, wanaunda timu isiyotarajiwa wanaposaidiana kupambana na majaribu ya kidijitali.
Kwa pamoja wanashughulikia masuala kama vile kuthibitisha ukweli wa taarifa, matumizi bora ya mitandao kwa ajili ya afya zao, na umuhimu wa faragha na usalama. Safari yao inawakutanisha na wadukuzi, walaghai na changamoto zinazowakabili katika ujuzi wao wa kidijitali.
Kudumisha utamaduni wa Noa Bongo Jenga Maisha Yako, kupitia mfululizo wa michezo ya redio ya DW iliyopata mafanikio makubwa – Elimu ya Kidijitali ni mkusanyiko wa hadithi za uvumbuzi, urafiki, na umuhimu wa elimu ya kidijitali katika ulimwengu unaobadilika kila mara.
Hadithi hizi zimeandikwa na waandishi wa Kiafrika na zinaletwa katika uhalisia na waigizaji kutoka bara lote la Afrika. Kila moja ya hadithi hizi tatu ina vipindi 10 vyenye urefu wa dakika 12.
Hadithi tatu za michezo ya redio ya DW kuhusu Elimu ya Kidijitali ni pamoja na:
Kisasi cha Mlaghai: Umeandikwa na James Muhando kutoka Kenya.
Panda Shuka: Mabadiliko ya Afya Yenye Tija: Umeandikwa na Marta Barroso kutoka Msumbiji.
Kuubadilisha Uongo kuwa Kweli: Umeandikwa na James Muhando kutoka Kenya.
Vipindi vinapatikana katika lugha ya Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamhara. Michezo ya Elimu ya Kidijitali inarushwa na DW pamoja na zaidi ya redio 300 washirika kote Afrika. Michezo yote hii inapatikana katika tovuti ya dw.com/Kiswahili/elimuyakidijitali na pia inajadiliwa katika majukwaa ya mitandao ya kijamii ya DW.