Mjumbe wa Marekani kuhusu Mashariki ya Kati yuko Beirut
19 Novemba 2024Matangazo
Kwa mujibu wa chanzo cha serikali, mjumbe huyo wa Marekani atakutana leo mchana na spika wa bunge Nabih Berri anayeliwakilisha kundi la Hezbollah katika mazungumzo hayo. Ziara ya Hochstein, Lebanon, inafanyika katika wakati ambapo jeshi la Israel limeripoti leo Jumanne, kwamba kiasi maroketi 40 yamefyetuliwa kutoka Lebanonkuelekea kaskazini na katikati mwa Israel na kusababisha watu wanne kujeruhiwa na vigae vya madirisha ya jengo lililolengwa na maroketi hayo. Jeshi la Israel pia limesema kundi la wanamgambo la Hezbollah ambalo linaungwa mkono na Iran, limefanya mashambulio hayo wakati kikosi cha wanaanga cha nchi hiyo kikiendesha mashambulizi makubwa dhidi ya mji wa Beirut, jana Jumatatu.